Mbadala wa Internet Download Manager (IDM)
Internet Download Manager (IDM) ni software rahisi kuitumia ambapo itakusaidia kupakua video kutoka kwenye website mbalimbali kama vile YouTube na mitandao mingine.
Pakua hapa software ya Internet Download Manager (IDM )
Hizi ni software ambazo hutolewa bure na hazina malipo yoyote ila zina mapungufu. Bado hazina sifa ya Internet Download Manager (IDM)
A. JDownloader
Hii ni software ambayo itakuwezesha kudownload mafile mbalimbali kutoka kwenye website mbalimbali ikiwemo picha, video,
music n.k
B. Free Download Manager (FDM)
Hii ni software ya bure ambayo utaweza kutumia bila kulipia. FDM inamuonekano kama wa Internet Download Manager kwahiyo hata feature baadhi zinaendana
C. EagleGet
Ni Software nzuri ambayo itakusadia kudownload mafile kutoka kwenye website mbali mbali kwa muda mfupi kutegemeana na speed ya internet yako. Ijaribu sasa
D. Internet Download Accelerator
Utakapotumia hii software, basi haina tofauti kabisa na Internet Download Manager. Ni rahisi kutumia hata kama hauna ujuzi wowote wa computer
E. FlashGet
Hii inafanana idea kama EagleGet lakini zinatofautiana kiutandaji hadi kimuonekano. Uzuri wa FlashGet ni bure na rahisi kutumia
F. Motrix
Hii ni software mbadala wa Internet Download Manager ambayo utakuwezesha kupakua video, picha, doc, music n.k kutoka kwenye website mbalimbali.
G. uGet Download Manager
Kupitia software hii utaweza kupakua mafile mbalimbali kutoka kwenye website mbalimbali kama vile Youtube n.k Ni rahisi kutumia hata kwa mtu ambaye hana ujuzi wowote wa computer
H. Ninja Download Manager
Ni software itakayokuwezesha kudownload software mbalimbali kutoka kwenye webiste kwa urahisi na kwa kuspeed kubwa kulingana na speed ya internet yako
I. Turbo Download Manager
Hii ni software ambayo inatolewa bure bila malipo ambayo itakuwezesha kupakua video, picha, music n.k kutoka kwenye website mbalimbali. Ni rahisi kutumia kwa mtu yoyote. Hii inafanya kazi kwenye Chrome kama extension
J. Xtreme Download Manager
katika software mbadala wa IDM basi hii ni nzuri kuliko zote. Nakushauri tumia hii software kwasababu ina feature zinazofanana na Internet Download Manager 78% kwahiyo utaweza kudownload files kutoka kwenye website mbalimbali kama vile unatumia IDM. Software hii ni bure yaani haina malipo
K. Aria2
Ni moja ya software ambayo ni mbadala wa Internet Download Manager ambayo itakuwezesha kupakua mafile kutoka kwenye website mbalimbali kwa urahisi zaidi. Hii ni software ya bure yaani haina malipo yoyote
Muhimu
Nimetumia Software nyingi kama mbadala wa Internet Download Manager lakini bado sijaona software ambayo inaweza kuifikia IDM 100% kwa ubora. IDM ni rahisi kutumia na pia ina uwezo wa ku-capture link yoyote na kuanza kudownload pale unapoiruhusu.
Post a Comment