Jinsi ya kuunlock Huawei E3372h-607 itumie mtandao wowote
Hii ni modem ambayo imefungwa ili iweze kutumia SIM Card ya mtandao mmoja tu kwahiyo ukiweka laini ya mtandao mwingine inakuomba SIM LOCK Code.
Kwa kutumia njia hii utaweza kufungua Huawei E3372h-607 na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka.
Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa modem.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hizi uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe modem yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock modem yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi
Namna ya kufungua Huawei E3372H-607 itumie mitandao yote
1. Install Huawei HiLink Drivers kwenye computer yako. Chomeka modem yako kwenye computer, hakikisha ina SIM Card ya mtandao mwingine
2. Run SBC master code calculator, chagua Huawei kisha weka IMEI namba ambazo zipo tarakimu 15. Funua mfuniko wa modem yako utaziona. Bonyeza Calculate, Copy Flash Code
3. Run Huawei E3372h-607 Unlocked Firmware kisha bonyeza Start.
4. Itaomba Password. Weka Flash code ulizozipata kwenye hatua namba 2. Iache mpaka imalizike kisha bonyeza Finish
6. Run Huawei E3372h-607 WEBUI unlocked Firmware kisha bonyeza start. Iache mpaka imalizike kisha bonyeza Finish
Hongera! Umefanikiwa kufungua modem yako ya Huawei E3372h-607 na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote
Post a Comment