Namna ya kurudisha files zilizofutwa kwenye computer, Flash drive, Hard disk na Memory Card (EaseUS Data Recovery Wizard)
Hii ni njia rahisi ambayo utaitumia kurudisha data zako zilizofutwa kama vile Audio, Picha, Video, Docx, Doc, Pdf n.k kwenye Computer, Hard disk, Flash drive au SD Card. Mtu yoyote ataweza kurudisha data zake hata kama hana ujuzi
Muhimu
Files zako zikifutika, usiweke files zingine kwenye hiyo device kwasababu zinaenda kufanya overwrite data zilizofutika na hivyo kufanya data zako zilizofutika kutozipata kirahisi.
Unapofanya Data recovery ni muhimu kuwa na External Hard disk au Flash drive kama Files zako zipo kwenye computer. Kama file zilizofutika zipo kwenye External Hard disk au flash drive, hifadhi data zako kwenye computer.
Jinsi ya kurudisha data zilizofutwa kwa kutumia EaseUS Data Recovery
1. Fungua EaseUS Data recovery. Chagua files gani unazohitaji kuzirudisha kisha bonyeza Next
2. Chagua partition unayotaka kurudisha data zako. Kama ni External Hard disk, Flash Drive au Memory card kisha bonyeza Scan
3. Bonyeza Deep Scan
4. Subiri mpaka zifike 100%. Itachukua kama dakika 14 tu kumalizika kwa process zote.
5. Weka tiki kwenye data unayotaka kuirudisha kisha bonyeza Recover
Mpaka hapa utakuwa umeweza kurecover File zako kwenye Computer, Hard disk, Flash drive au Memory Card (SD Card)








Post a Comment