Jinsi ya kuunlock Huawei E3372h-153 Orange 4G LTE

Hii ni modem iliyofungwa ili iweze kutumia SIM Card ya mtandao mmoja tu na ukiweka SIM Card ya mtandao mwingine inaomba SIMLOCK Code

Kwa kutumia njia hii, utaweza kuunlock Huawei E3372h-153 Orange na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote.

Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa modem.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hizi uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe modem yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock modem yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi

Namna ya kuunlock Huawei E3372h-153 Orange itumie mtandao wowote
1. Install Huawei Driver kwenye computer yako Huawei_DataCard_Driver_6.00.08.00_Setup & Mobile Broadband HL Service

Soma
Run DC Unlocker 2 Client as administrator. Bonyeza kwenye magnifying glass, ikileta taarifa za modem yako. Anzia hatua namba 1, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10, 11 & 12

Isipoleta taarifa za modem yako anzia hatua 1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10, 11 & 12

2. Fungua Modem yako ya Huawei E3372h-153 4G Orange kwa Screw Driver. Kisha piga shot kwa kugusanisha hizi point huku umechomeka kwenye computer yako. Itadetect na COM Port za modem yako itaonekana. Ikifunguka browser ya router yako ifunge.

3. Run Balong USB Downloader kisha bonyeza Detect. Com Port ya Modem yako itaonekana. Bonyeza kwenye vidoti vitatu kwenye Load 

Chagua usbloader.bin kisha bonyeza Open

Bonyeza Load. ikimalizika, funga Balong USB Downloader Tool

4. Run SBC Code Calculator, Bonyeza kwenye Huawei Tab, weka IMEI za modem yako kisha bonyeza kwenye Calculate kupata Flash Code
5. Run Huawei E3372h-153 Orange Downgrade Firmware kisha bonyeza start. Itaomba password, weka za flash code ulizozipata hatua namba 4 kisha bonyeza Ok. Iache mpaka imalizike kisha bonyeza Finish

6. Run DC Unlocker 2 Client as administrator. Bonyeza kwenye magnifying glass. Utaletewa taarifa za modem yako. Mwisho mwa hizo taarifa, weka hizi code AT^NVRDEX=50503,0,128 kisha bonyeza ENTER kwenye keyboard ya computer yako.

Ikigoma, fanya hivi
- Funga Huawei mobile partner dashboard
- Funga Tab ya Huawei dashboard kwenye browser yako
- Chomoa modem yako kwenye computer kisha chomeka tena. Endelea na hatua namba 5

7. Utaletewa NV Harsh code. Kama hivi

Nitumie NV Harsh Code kwa SMS, WhatsApp & Telegram +255767434014 kupata NCK Code

8. Run Huawei E3372h-153 Orange Upgrade firmware. Bonyeza Start kisha Next iache mpaka imalize. Bonyeza Finish

9. Chomoa modem yako kwenye computer. Weka SIM Card ya mtandao mwingine kisha chomeka kwenye computer
10. Itafunguka browser yenye address hii "192.168.8.1"
11. Weka User name na "Password" kisha bonyeza "Log In" ambazo ni admin kwa zote

12. Weka NCK code ulizotumiwa na timu ya Fahusvera kisha bonyeza "Apply"
Hongera! Umefanikiwa kuunlock Huawei E3372h-153 Orange na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaotaka
Tags: Jinsi ya kuunlock E3372h-153 4G LTE Orange itumie mtandao wowote, jinsi ya kuunlock Huawei E3372h-153 4G LTE  Orange itumie yote, how to unlock E3372h-153 Orange, how to unlock Huawei E3372h-153 Orange, how to unlock E3372h-153 4G LTE , how to unlock Huawei E3372h-153 4G LTE, Download firmware for E3372h-153 Orange, E3372h-153 Orange Firmware

Read more >>>>> Namna ya kuunlock Alcatel Onetouch X225S itumie mitandao yote

No comments