Jinsi ya kuunlock Huawei E303 MTN Uganda itumie mitandao yote
Ni modem ambayo imetolewa na kampuni ya simu MTN uganda ambayo itakutaka utumie SIM Card ya mtandao mmoja tu kwahiyo ukitaka kuweka laini ya mtandao mwingine inakuomba SIMLOCK Code.
Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa modem.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hizi uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe modem yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock modem yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi
Hii ni modem ya Hi-link ambapo Com Port zake hazionekani kwenye Computer Management >>> Port (Com & LPT) kwahiyo ili uwezeshe, fuata njia hii. Namna ya kuwezesha Com Port za Huawei E303 Hilink MTN Uganda
Namna ya kuunlock Huawei E303 MTN Uganda itumie mitandao yote
1. Chomeka modem kwenye computer ikiwa na laini ya mtandao mwingine. Ikifungua dashboard, funga.
2. Run SBC Code Calculator. Weka IMEI za modem zako, zipo 15 digits. Bonyeza calculate kupata Flash code (Hizi ndizo zinazohitajika)
3. Run Huawei E303 Hilink MTN Unlocked Firmware. Bonyeza Start, ikiomba password. Weka za Flash Code kisha bonyeza OK. Ikimaliza, Bonyeza Finish
4. Run Huawei Modem Code Writer. Bonyeza kwenye Please Select Com Port
5. Bonyeza kwenye Detect kisha chagua COM Port ya modem yako
6. Bonyeza Accept
7. Bonyeza Unlock Modem
8. Weka Unlock Code ambazo ni 8 digits kisha bonyeza OK
Hongera! Umefanikiwa kuunlock modem ya Huawei E303 MTN Uganda na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule.
Post a Comment