Jinsi ya kuunlock Huawei E5573s-606 itumie mitandao yote

Hii ni router ambayo inakutaka utumie SIM Card ya mtandao mmoja tu kwahiyo unapotaka kutumia SIM Card ya mtandao mwingine inakuomba SIM LOCK Code.

Kwa kushirikiana na team ya Fahusvera, utaweza kuunlock router yako ya E5573s-606 itumie mitandao yote popote ulipo

Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa router tu.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hizi uta-brick router yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe router yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock router yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi

Namna ya kuunlock Huawei E5573s-606 itumie mitandao yote
1. Fungua router yako kwa screw driver. Piga short motherboard kwa kuunganisha point A & B kisha unganisha router na computer kwa USB Cable huku umeunganisha point A & B. Utaona router yako imekuwa detect kwenye computer. 

Install FC Serial Driver driver na Huawei DataCard Driver kwenye computer yako

2. Run Balong USB Downloader. Bonyeza Detect utaona com port ya router yako imeonekana. Bonyeza vidoti vitatu, chagua usbloaderE5573s.bin kisha bonyeza Load. Iache mpaka imalize yenyewe. Funga Balong USB Downloader

3. Run Huawei Master Code Calculator, Bonyeza Huawei Tab, weka IMEI za modem yako kisha bonyeza kwenye Calculate kupata Flash Code

4. Run Huawei E5573s-606 Downgrade Firmware kisha bonyeza start. Itaomba password, weka za flash code ulizozipata hatua namba 4 kisha bonyeza Ok. Iache mpaka imalizike kisha bonyeza Finish

5. Run DC Unlocker 2 Client as administrator. Bonyeza kwenye magnifying glass. Utaletewa taarifa za modem yako. Mwisho mwa hizo taarifa, weka hizi code AT^NVRDEX=50503,0,128 kisha bonyeza ENTER kwenye keyboard ya computer yako.

Ikigoma, fanya hivi
- Funga Huawei mobile partner dashboard
- Funga Tab ya Huawei dashboard kwenye browser yako
- Chomoa modem yako kwenye computer kisha chomeka tena. Endelea na hatua namba 5

6. Utaletewa NV Harsh code. Kama hivi. Nitumie NV Harsh Code kwa SMS, WhatsApp & Telegram +255767434014 kupata NCK Code

7. Run Huawei E5573s-606 Upgrade firmware. Bonyeza Start kisha Next iache mpaka imalize. Bonyeza Finish

8. Chomoa router yako kwenye computer. Weka SIM Card ya mtandao mwingine kisha unganisha na Wi-FI
10. Itafungua browser yenye address hii "192.168.8.1"
11. Weka User name na "Password" kisha bonyeza "Log In" ambazo ni admin kwa zote

12. Weka NCK code ulizotumiwa na timu ya Fahusvera kisha bonyeza "Apply"

 
Hongera! Umefanikiwa kuunlock Huawei E5573s-606 na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote
Tags: Jinsi ya kuunlock E5573s-606 itumie mtandao wowote, namna ya kuunlock Huawei E5573s-606 itumie mitandao yote, jinsi ya kufungua Huawei E5573s-606 itumie mitandao yote, namna ya kufungua E5573s-606 itumie mtandao wowote, how to unlock E5573s-606, how to unlock Huawei E5573s-606, download Huawei E5573s-606 firmware, download E5573s-606 firmware

No comments