Jinsi ya kuunlock E303s-2 Hilink Vodacom Tanzania

Hii ni modem ya Huawei E303s-2 Vodacom Tanzania ambayo inatumia SIM Card wa Vodacom Tanzania tu kwahiyo ukiweka SIM card ya mtandao mwingine inakuandikia Invalid SIM Card. Hii ni modem ya E303s-2 ambayo inafungukia kwenye browser kama vile Chrome, Firefox, Opera n.k

Kwa kutumia njia hii utaweza kuunlock modem yako ya E303s-2 Hilink Vodacom Tanzania na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka

Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa modem yako.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hii uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe modem yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock modem yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi

Nanma ya kuunlock Huawei E303s-2 Hilink Vodacom Tanzania

1. Weka SIM Card ya mtandao mwingine kisha chomeka modem yako kwenye computer. Ikifunguka browser ya modem yako ifunge

2. Run Huawei Universal Master Code, bonyeza Huawei weka IMEI number ya modem yako kisha bonyeza Calculate kupata Flash Code. Nukuu Flash Code

3. Run Huawei E303s-2 Hilink Unlocked Firmware. Bonyeza Start
4. Ikiomba Password, weka za Flash Code ulizozipata kwenye Universal Master code calculator kisha bonyeza OK. Iache mpaka imalize, ikimaliza bonyeza Finish

Hongera! Mpaka hapa utakuwa umefanikiwa kuunlock E303s-2 Hilink Vodacom Tanzania na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka

Read more >>>>  Namna ya kuunlock Huawei E303s-2 Non Hilink Vodacom Tanzania itumie mitandao yote

No comments