Namna ya kuzuia Matangazo kwenye Computer

Unapokuwa unaperuzi mtandaoni, utakutana na matangazo mengi sana kwenye website au blog unazotembelea zikiwa kwenye mfumo wa Video, GIF au Picha. 

Huwa inaleta kero mpaka unaamua kutotembelea baadhi ya website kwa usumbufu wa matangazo. Adguard ni software ambayo itakusaidia
kuzuia matangazo ya aina yoyote yakiwemo Picha, GIF, Video n.k na pia ina feature ya "Parental Control ambayo itakuwezesha Kublock website zote zenye viashiria vya ngono kwenye browser yoyote kama vile Chrome, Mozilla Firefox, UC Browser, Opera mini n.k kwenye computer yako.

Jinsi ya kuzuia website zenye viashiria vya ngono kwa kutumia Adguard
Hii itazuia matangazo yote pamoja na website zake zenye viashiria vya ngono

Itakuhitaji u-set Parental Control kwenye Adguard

1. Fungua Adguard Bonyeza Settings

2. Bonyeza Parental Control, Enable Parental Control > weka tiki kwenye Safe Search na Block executable file downloads

Kama unatumia Search Engine ya Google Unaweza kuweka Safe Search kwenye Google Chrome na browser zingine kama Firefox, Brave, Operamin n.k
- Ingia Google angalia upande wa kulia utaona neno Settings >Hide Explicit results

Requirements
* Adguard Ads Blocker (With life time Serial Key)
* Computer

Muhimu
Kabla ya kuinstall Adguard ingia kwenye hii website Filehippo au Savefrom
Hizi ni website zenye matangazo kwahiyo ukishainstall Adguard na ukaingia kwenye hizi website hautaweza kuona matangazo ya aina yoyote yale

Jinsi ya kuzuia matangazo (Ads) kwenye computer. Njia hii itazuia matangazo ya aina yoyote ukiwa unatumia browser yoyote ile
1. Install Adguard kwenye computer yako kisha ifungue na hakikisha imeandikwa "Protection is Enabled"

Hapo hautaona matangazo ya aina yoyote kwenye computer yako. Kwenye Taskbar itakuwa inaonekana kama hivi

Jinsi ya kuzuia Video za YouTube kutocheza mpaka uziruhusu (How to turn off Autoplay on YouTube)

 

Kwa wale wanaotumia Chrome, unaweza kuzuia Autoplay video, GIF, na Animation ukiingia kwenye Youtube. Ukifungua video yoyote ya YouTube itaanza kucheza yenyewe (Kwa wale wanaotaka wasitumie bundle sana la Internet). Kwa kutumia hizi extensions za Chrome utaweza kufungua video yoyote ya youTube na ukairuhusu kucheza au kutocheza. 

Hii inatumika kwa website zote zenye Video, GIF na Animation zinazoplay Zenyewe na hizi software ni bure hazina malipo yoyote. Tumia link hizi kuinstall AutoplayStopper na Animation Policy kwenye Chrome au Ingia Chrome web store  kisha andika AutoplayStopper au Animation Policy

Jinsi ya kuzuia matangazo ya internet kwenye Chrome 

Jinsi ya kuzuia matangazo ya internet kwenye Opera Browser

Jinsi ya kuzuia matangazo ya internet kwenye UC Browser

Tags:  Jinsi ya kuzuia matangazo kwenye internet, zuia matangazo online, namna ya kuzuia matangazo unapoperuzi mtandaoni, jinsi ya kuzuia matangazo mtandaoni kwenye computer, zuia matangazo mtandaoni, njia rahisi ya kuzuia matangazo ya internet, njia rahisi ya kuzuia matangazo mtandaoni, zuia matangazo yanayojitokeza kwenye internet, njia rahisi ya kuzuia matangazo ya internet kwenye computer, njia rahisi ya kuzuia matangazo ya internet kwenye Laptop, njia rahisi ya kuzuia matangazo ya internet kwenye desktop, Laptop, computer, zuia website zenye matangazo mengi, zuia matangazo kwenye blog, zuia matangazo kwenye website, zuia blog zenye matangazo mengi

No comments