Namna ya kuunlock E303 Airtel Tanzania itumie mitandao yote
Hii ni modem ambayo imefungwa ili uweze kutumia SIM Card ya mtandao mmoja tu kwahiyo ukijaribu kutumia laini ya mtandao mwingine haisomi.
Kwa kutumia njia hii utaweza kufungua modem ya Huawei E303 Airtel Hilink na utaweza kutumia laini ya mtandao wowote ule unaoutaka
Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa modem.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hizi uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe modem yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock modem yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi
Jinsi ya kuunlock Huawei E303 Hilink Airtel Tanzania
1. Install Huawei Mobile Partner kisha funga dashboard.
2. Run SBC Code Calculator > bonyeza Huawei, weka IMEI number kisha bonyeza Calculate ili kupata Flash Code. Kupata IMEI Number, fungua mfuniko wa modem yako utaziona. Zipo tarakimu 15
3. Run E303 Hilink Airtel Unlocked Firmware. Itaomba Password, weka Flash Code kisha bonyeza OK. Subiri mpaka imalize. Ikimaliza chomoa na chomeka tena ikiwa SIM Card ya mtandao wowote
Hongera! Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuunlock E303 Airtel Tanzania na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote. Enjoy!
Post a Comment