Namna ya kuunlock ZTE MF180 Airtel Tanzania itumie mitandao yote
Hii ni modem ya ZTE MF180 ya kampuni ya Airtel ambayo imefungwa ili iweze kutumia SIM Card ya mtandao mmoja tu kwahiyo ukijaribu kutumia SIM Card ya mtandao mwingine, inakataa kusoma.
Kwa kutumia njia hii utaweza kuunlock ZTE MF180 na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote
Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa modem yako.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hii uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe modem yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock modem yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi
Jinsi ya kuunlock ZTE MF180 Airtel Tanzania itumie mtandao wowote
A. Chomeka modem yako ikiwa na SIM Card ya mtandao wowote tofauti na Airtel kwenye Computer.
B. Install ZTE MF180 driver kwenye computer
C. Ikifungua, Dashboard. Funga Dashboard ya modem yako.
D. Run ZTE MF180 Airtel unlocked firmware, bonyeza start, bonyeza next. Iache mpaka imalize. Ikimaliza, bonyeza Finish.
Post a Comment