Jinsi ya kuunlock Huawei E153u-1 Tigo Tanzania

Hii ni modem ya Huawei E153u-1 Tigo ambayo inatumia SIM Card wa Tigo Tanzania tu kwahiyo ukiweka SIM card ya mtandao mwingine inakuandikia Invalid SIM Card

Kwa kutumia njia hii utaweza kuunlock modem yako ya E153u-1 Tigo Tanzania na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka

Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa modem yako.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hii uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe modem yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock modem yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi

Namna ya kuunlock Huawei E153u-1 Tigo Tanzania itumie mtandao wowote
1. Weka SIM Card ya mtandao mwingine kisha chomeka modem yako kwenye computer
2. Install dashboard ya modem yako ili kuinstall drivers za modem yako
3. Baada ya kuinstall, itafunguka dashboard ya modem yako. Ifunge
4. Run Universal Master Code, Bonyeza Huawei Tab kisha weka IMEI za modem yako ambazo ni tarakimu 15, bonyeza Calculate kupata Flash Code. Nukuu Flash Code
5. Run E153u-1 Tigo Unlocked Firmware, bonyeza Start, Iitaomba Password. Weka za Flash Code kisha bonyeza OK, iache mpaka imalize yenyewe. Ikimaliza bonyeza Finish

6. Run Huawei Modem Code Writer. Bonyeza kwenye Please Select Com Port

7. Bonyeza kwenye Detect kisha chagua COM Port ya modem yako

8. Bonyeza Accept

9. Bonyeza Unlock Modem
 
10. Weka Unlock Code ambazo ni 8 digits kisha bonyeza OK

Hongera! Mpaka hapa utakuwa umefanikiwa kuunlock E153u-1 Tigo Tanzania na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka.

Tags: Jinsi ya kuunlock E153u-1 Tigo Tanzania, Jinsi ya kuunlock Huawei E153u-1 Tigo Tanzania, namna ya kufungua E153u-1 Tigo Tanzania itumie mitandao yote, namna ya kufungua Huawei E153u-1 Tigo Tanzania, how to unlock E153u-1 Tigo Tanzania, how to unlock Huawei E153u-1 Tigo Tanzania, Download E153u-1 Tigo Tanzania firmware, Download E153u-1 Tigo Firmware, Download firmware for E153u-1 Tigo Tanzania, Download Huawei E153u-1 Firmware

 

No comments