Jinsi ya kuunlock Huawei Mifi E5573s-156 MTN

Hii ni router ambayo imefungwa na mtandao wa MTN ili uweze kutumia laini ya mtandao mmoja na unapojaribu kutumia SIM Card ya mtandao mwingine inakuomba SIMLOCK Code.

Kwa kutumia njia hii, utaweza kuunlock Huawei E5573s-156 MTN na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule.

Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa router.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hizi uta-brick router yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe router yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock router yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi

Namna ya kuunlock Huawei E5573s-156 MTN itumie mitandao yote
1. Install Huawei Drivers, Mobile Partner na FcSerialDrv kwenye computer yako
Ingia kwenye Windows Explorer. Right click kwenye This Computer au My computer >>> Manage >>> Device Manager
>>> Ports (COM & LPT). Ili uingie kwenye computer computer management
a. Right click kwenye HUAWEI Mobile Connect - 3G PC UI Interface kisha bonyeza Update Driver Software
b. Bonyeza Browse my Computer for driver software kisha bonyeza browse.
c. Bonyeza kwenye Browse
d. Itafunguka Windows, chagua folder ambalo lina drivers kulingana na bit ya windows yako. Ya kwangu ni Windows 10 bit 32/86 kwahiyo nachagua
X86 kisha bonyeza OK. Jinsi ya kutambua Windows Bit ya computer yako
e. Kisha bonyeza Next
f. Itaanza kuinstall Drivers. Ikigoma, hasa kwa wale wanaotumia Bit x64 itakulazimu u-disable Driver signature Enforcement kwenye computer yako. Jinsi ya kudisable Driver Signature Enforcement. Ikimaliza bonyeza kwenye Close. Fanya hivyo tena kwenye kuinstall FcSerialDrv

2. Connect Huawei Mifi router yako na computer kwa USB Cable
3. Fungua huawei Master code calculater, weka IMEI kisha bonyeza calculate kupata Flash Code (Kuzipata IMEI, Funua mfuniko wa router utaziona tarakimu 15)
4. Run Huawei E5573s-156 MTN Downgrade Firmware kisha bonyeza Start. Ikiomba Password, weka za Flash Code. Iache mpaka imalize yenyewe. Ikimaliza, bonyeza "Finish"
Ikileta ujumbe wa Error 10: Find port failed. Fungua kwenye folder la Driver >>>>>> Install 1 Error Code 10 >>>>>>>
run USB_E5573_USB_controller au Error Code 10 kisha endelea na hatua namba 4.
5. Run DC Unlocker Client as administrator kisha bonyeza Magnifying Glass Button. Utaletewa taarifa za router yako
Ikigoma, fanya hivi
- Funga Huawei mobile partner dashboard
- Funga Tab ya Huawei dashboard kwenye browser yako
- Chomoa router yako kwenye computer kisha chomeka tena. Endelea na hatua namba 5

6. Mwisho wa taarifa za router yako kwenye DC Unlocker Client. Weka code hizi AT^NVRDEX=50503,0,128 kisha bonyeza ENTER kupata NV Hash Code

7. Utapata NV Hash Code kama inavyoonekana kwenye picha
8. Nitumie NV Hash Code kwa SMS, WhatsApp & Telegram +255767434014 Kupata NCK Code.
9. Run Huawei E5573s-156 MTN Upgrade Firmware kisha Bonyeza Start. Iache mpaka imalize yenyewe kisha bonyeza "Finish"
10. Chomoa router yako. Weka SIM Card ya mtandao mwingine kisha iwashe
11. Unganisha WIFI na computer yako. Itafungua browser yenye address hii 192.168.8.1 kwenye computer yako
12. Weka User name na Password (admin kwa zote) kisha bonyeza Log In
13. Weka NCK Code nilizokutumia kisha bonyeza Apply
Hongera! Umefanikiwa kuunlock Huawei E5573s-156 MTN na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaotaka.
Tags: Jinsi ya kuunlock E5573s-156 MTN itumie mtandao wowote, namna ya kuunlock Huawei E5573s-156 MTN itumie mitandao yote, namna ya kufungua Huawei E5573s-156 MTN, jinsi ya kufungua E5573s-156 MTN, jinsi ya kuunlock Huawei E5573s-156 itumie mitandao yote, namna ya kuunlock E5573s-156 itumie mtandao wowote, how to unlock Huawei E5573s-156, how to unlock E5573s-156, how to unlock E5573s-156 MTN, how to unlock Huawei E5573s-156 MTN, download Huawei E5573s-156 MTN firmware, download E5573s-156 firmware, jinsi ya kuunlock router ya Africel E5573s-156 itumie mitandao yote, namna ya kufungua router ya E5573s-156 MTN itumie mitandao yote

No comments