Jinsi ya kuunlock E303h-1 MTN itumie mitandao yote

Hii ni modem ya Huawei E303h-1 MTN ambayo inatumia SIM Card wa MTN tu kwahiyo ukiweka SIM card ya mtandao mwingine inakuandikia Invalid SIM Card.

Kwa kutumia njia hii utaweza kuunlock modem yako ya E303h-1 MTN na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka

Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa modem yako.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hii uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe modem yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock modem yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi

Namna ya kuunlock Huawei E303h-1 MTN itumie mitandao yote
1. Weka SIM Card ya mtandao mwingine kisha chomeka modem yako kwenye computer
2. Install dashboard ya modem yako ili kuinstall drivers za modem yako
3. Baada ya kuinstall, itafunguka dashboard ya modem yako. Ifunge
4. Run Universal Master Code, Bonyeza Huawei Tab kisha weka IMEI za modem yako ambazo ni tarakimu 15, bonyeza Calculate kupata Flash Code. Nukuu Flash Code

5. Run E303h-1 MTN Unlocked Firmware, bonyeza Start. Itaanza ku-find Port kisha itaomba Password. Weka za Flash Code kisha bonyeza OK, iache mpaka imalize yenyewe. Ikimaliza bonyeza Finish

Hongera! Mpaka hapa utakuwa umefanikiwa kuunlock E303h-1 MTN na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka.

Tags: Jinsi ya kuunlock E303h-1 MTN, Jinsi ya kuunlock Huawei E303h-1 MTN, namna ya kufungua E303h-1 MTN itumie mitandao yote, namna ya kufungua Huawei E303h-1 MTN, how to unlock E303h-1 MTN, how to unlock Huawei E303h-1 MTN, Download E303h-1 MTN firmware, Download E303h-1 MTN Firmware, Download firmware for E303h-1 MTN, Download Huawei E303h-1 Firmware.

Read More >>>> Namna ya kuunlock router R6601 Halotel Tanzania
 

No comments