Jinsi ya kuunlock M028AT TTCL Tanzania Itumie mitandao yote
Hii ni 4G Mifi router ya kampuni ya TTCL inayokutaka utumie SIM Card ya mtandao mmoja tu TTCL na ukiweka laini ya mtandao mwingine inakuomba PH-NET PIN
Kwa kutumia njia hii, utaweza kuunlock router yako na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka
Mahitaji
- M028AT TTCL Flash tool
- M028AT TTCL unlocked firmware
- M028AT Drivers
- USB Cable
Namna ya kuunlock M028AT TTCL Tanzania itumie mitandao yote
1. Install M028AT TTCL drivers kwenye computer yako. Ikimalizika bonyeza Finish
2. Weka laini ya mtandao mwingine au usiweke. Kisha washa
3. Chomeka router yako kwenye computer kwa USB Cable
4. Run M028AT TTCL Tanzania unlocked firmware. Bonyeza start. Iache mpaka imalize kisha bonyeza Finish
5. Chomoa router yako kwenye computer, toa battery. Weka SIM Card ya mtandao mwingine. Kisha washa
Hongera! Umefanikiwa kuunlock M028AT TTCL Tanzania na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka
Read more >>>>> Namna ya kuunlock Alcatel X230E Airtel Tanzania itumie mitandao yote



Post a Comment