Jinsi ya kuunlock Vodafone 300 Vodacom Tanzania
Hii ni simu ya promotion ambayo imefungwa SIM 1 ili uweze kutumia mtandao mmoja tu kwahiyo Ili uweze kupata internet ya 3G (H+) kwenye simu yako lazima SIM 1 uweke laini ya mtandao wa kampuni husika.
Faida baada ya kuunlock vodafone VFD 300
- Utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaotaka
- Utaweza kupata internet ya H+ ukiwa na laini ya mtandao wowote ule
- Utaweza ku-root
Mahitaji
- Vodafone 300 Unlocked Firmware:
Size: 39.76 MB
- Computer
- Splash Flash Tool
- Mediatek VCOM USB Drivers
- Simu ya Vodafone VFD 300
- USB Cable
Namna ya kuunlock Vodafone VFD 300 itumie mtandao wowote. Hatua kwa hatua
1. Download Vfd 300 unlocked Firmware kisha extract kwenye computer yako. Tumia Winrar kuextract firmware yako
> Install Mediatek USB VCOM Drivers
2. Download SP Flash Tool na launch kwenye computer yako.
> Weka Download Only
> Bonyeza Choose kwenye Scatter Loading File
4. Bonyeza Download button. Zima simu, chomoa battery kisha rudishia tena battery. Connect USB Cable kwenye computer. Itaanza kuupdate firmware yenyewe.
5. Italeta ujumbe wa tiki "Download Ok". Toa USB cable, Toa na weka battery tena kisha washa simu yako.
Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuunlock simu yako ya VFD 300 na utaweza kutumia mtandao wowote ule kwenye SIM 1 Slot.
Muhimu
- Hakikisha simu yako ina chaji 50%
- Usiguse simu wakati wa kuunlock simu yako au computer
- Hakikisha Computer yako ina chaji ya kutosha kama unatumia Laptop
Post a Comment