Jinsi ya kuunlock E3131 Zantel Tanzania itumie mitandao yote

Hii ni modem iliyofungwa ili iweze kutumia laini ya mtandao mmoja tu yaani Zantel na unapojaribu kutumia laini ya mtandao mwingine inakataa kutambua SIM Card za mitandao mingine.

Hii ni njia ambayo itakuwezesha kuuunlock modem yako ya Huawei E3131 na utaweza kutumia laini za mitandao yote

Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa modem.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hizi uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe modem yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock modem yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi

Namna ya kuunlock Huawei E3131 Zantel itumie mitandao yote
1. Chomeka modem yako ya Huawei E3131 kwenye computer yako ikiwa na SIM Card ya mtandao mwingine. Ikifungua dashboard, basi ifunge.

2. Run Huawei Code calculator. Weka IMEI za modem yako ili kupata Flash code

3. Run E3131 Unlocked Firmware kisha bonyeza "Start". Itakuomba Password, weka za Flash Code ulizozipata kwenye hatua namba 2. Iache mpaka imalize hatua zote


Ikimaliza chomoa na chomeka tena modem yako. Hongera mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kufungua modem yako ya Zantel na utaweza kutumia SIM Card
ya mtandao wowote ule.

Tags:  Jinsi ya kuunlock E3131 Zantel Tanzania itumie mtandao wowote, namna ya kufungua E3131 Zantel Tanzania, jinsi ya kuunlock Huawei E3131, namna ya kufungua Huawei E3131, jinsi ya kuunlock modem ya E3131 Zantel Tanzania itumie mitandao yote, namna ya kuunlock modem ya Zantel E3131, how to unlock E3131 Zantel Tanzania, how to unlock Huawei E3131 Zantel Tanzania, how to unlock E3131, how to unlock  Huawei   E3131

No comments