Namna ya kuunlock E3372h-153 Tigo Tanzania
Hii ni modem ya tigo ilifungwa ili iweze kutumia mtandao mmoja tu kwahiyo ukiweka SIM Card ya mtandao mwingine inakuomba SIM LOCK Code
Kwa njia hii utaweza kuunlock modem ya Huawei E3372h-153 (Firmware Version 22.200.09.00.787 na web UI Version 17.100.11.01.787) iweze kutumia SIM Card ya mtandao wowote
Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa modem.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hizi uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe modem yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock modem yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi
Jinsi ya kuunlock Huawei E3372h-153 Tigo Tanzania itumie mtandao wowote
1. Chomeka modem yako ikiwa na SIM Card ya mtandao mwingine kisha install Huawei DataCard driver kwenye computer yako
2. Run Universal Master Code, weka IMEI ya modem yako ambazo zipo digit 15, bonyeza Huawei, weka IMEI kisha bonyeza button ya Calculate ili kupata Flash Code. Kumbuka hapa tunahitaji Flash Code tu.
3. Run Transitional Firmware. Bonyeza Start, Itakuomba password, weka za flash code kisha bonyeza OK, iache mpaka imalize. Ikimaliza bonyeza Finish
4. Run DC Unlocker as administrator, Chagua "Huawei modems" kwenye Select Manufacturer na
"Auto Detect" (Recommended) kwenye Select model kisha Bonyeza Magnifying
Glass button.
5. Utaletewa taarifa za modem yako. Mwisho mwa hizo taarifa, weka hizi code AT^NVRDEX=50503,0,128 kisha bonyeza ENTER kwenye keyboard ya computer yako.
- Funga Huawei mobile partner dashboard
- Funga Tab ya Huawei dashboard kwenye browser yako
- Chomoa modem yako kwenye computer kisha chomeka tena. Endelea na hatua namba 5
6. Utaletewa NV Harsh code. Kama hivi, nitumie NV Harsh Code kwa SMS, WhatsApp & Telegram +255767434014 kupata NCK Code
7. Rudi kwenye DC Unlocker. Bonyeza Magnifying glass, italeta details za modem yako. Mwisho wa details andika command hizi AT^SFM =1 kisha bonyeza Enter kwenye keyboard ya computer yako
8. Run Modified Firmware, bonyeza start >>> Next. Kama itaomba Password. Weka za Flash Code ulizozipata kwenye hatua namba 2, iache mpaka imalize, ikimaliza bonyeza Finish
9. Rudi kwenye DC Unlocker, Bonyeza Magnifying button. Itakuletea details zote za modem yako mwisho wa taarifa weka command hizi AT^NVWREX=8268,0,12,1,0,0,0,2,0,0,0,A,0,0,0 kisha bonyeza Enter kwenye keyboard ya Computer yako.
10. Chomoa modem yako kwenye computer. Weka SIM Card ya mtandao mwingine kisha chomeka tena kwenye computer
11. Itafunguka browser yenye address hii "192.168.8.1"
12. Weka User name na "Password" kisha bonyeza "Log In" ambazo ni admin kwa zote
Hongera! Umefanikiwa kuunlock Huawei E3372h-153 Tigo Tanzania na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaotaka
Kama utataka kuweka salio, kupiga simu au kutuma meseji kupitia modem yako. Basi, tumia Huawei Mobile Partner
Tags: Jinsi ya kuunlock Huawei E3372h-153 Tigo Tanzania itumie mtandao wowote, namna ya kuunlock E3372h-153 Tigo Tanzania itumie mitandao yote, namna ya kufungua Huawei E3372h-153 Tigo Tanzania itumie mtandao wowote, jinsi ya kufungua E3372h-153 Tigo Tanzania itumie mitandao yote, namna ya kufungua modem ya Tigo Huawei E3372h-153 itumie mtandao wowote, jinsi ya kuunlock modem ya Huawei E3372h-153 Tigo Tanzania itumie mitandao yote, how to unlock Huawei E3372h-153 Tigo Tanzania, how to unlock E3372h-153 Tigo Tanzania, download Huawei E3372h-153 Tigo Tanzania firmware, download E3372h-153 Tigo Tanzania firmware
Post a Comment