Namna ya kuunlock D-link DWM 157 itumie mtandao wowote
Hii ni modem ya 4G ambayo imefungwa ili iweze kutumia SIM Card ya mtandao mmoja tu kwahiyo kwa kutumia njia hii itakusaidia ku-unlock modem ya D-link DWM 157 ili uweze kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule. Baada ya kuunlock, utaweza kutumia laini ya mtandao wowote ule unaotaka.
Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa modem.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hizi uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe modem yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock modem yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi
Jinsi ya kuunlock D-link DWM 157 Zantel itumie mitandao yote
1. Download D-link DWM 157 Unlocked Firmware kisha extract kwenye computer yako. Tumia Winrar au 7-Zip kuextract Unlocked firmware kwenye computer yako.
2. Chomeka modem yako kwenye computer, iache mpaka imalize kuinstall drivers zote. Kisha funga Dashboard ya modem yako kwasababu itashindwa kuwa unlocked. Weka laini ya mtandao mwingine tofauti na wa mtandao husika
3. Launch Dlink 157 unlocked firmware
> Tiki kwenye "I accept the agreement"
> Bonyeza "Next"
4. Itaanza ku-update firmware kwahiyo iache mpaka imalize. Usiichomoe au kuitingisha na hakikisha computer yako ina charge ya kutosha.
5. Mwisho itaileta ujumbe "Firmware updated successfully" kisha bonyeza "Finish"
Hongera! Mpaka hapa utakuwa umeweza kuunlock modem yako ya D-link 157 Zantel Tanzania na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule.
Post a Comment