Jinsi ya kurudisha Picha zilizofutwa kwenye Computer, Flash Drive, Hard disk na Memory Card

Kama umefuta Photos/image kwa bahati mbaya au zimeharibiwa na Virus kwenye Computer, Hardisk, Flash Drive au SD Card (memory card) basi uwezekano wa kuzipata ni 100% hata kama ni Picha za zamani, halafu ukaitumia kifaa chako kuweka data zingine. Njia hii ni rahisi na mtu yoyote anaweza kuitumia kurudisha Photos hata kama hana ujuzi wowote wa computer.

Kama ni SD Card yaani Memory Card umefuta (delete au format), ume-format au ume-reset simu ikafuta Picha zako zote basi chomoa Memory Card na uweke kwenye TransFlash Adapter

Muhimu
- Software hii siyo kama itarudisha Photos tu bali Video, Music, Document (PDF, DOC n.k)
- Usiweke vitu vipya vingine kwenye Partition ya Computer ambayo data zimefutwa, Hard disk, Flash Drive au SD Card
- Kwa matokeo mazuri kama Photos zako zipo kwenye computer, tumia Flash Drive, Memory Card au Hard disk kuhifadhi data zako kipindi cha kufanya Data Recovery.

Kama data zako zipo kwenye SD Card, Flash Drive au External Hard disk, tumia computer yako kuhifadhi picha zako

Mahitaji
- MiniTool Power Data Recovery
- Computer
- SD Card, Flash Drive au Hard disk (Kama image zako zipo kwenye computer ili kupata matokeo mazuri)

Hatua kwa hatua namna ya kurudisha picha zilizofutwa kwenye SD Card, Flash Drive, Computer au Harddisk

1. Chomeka Flash Drive, Harddisk, au SD Card kwenye Computer kisha fungua MiniTool Power Data Recovery. Chagua Option inayofaa kwako. Mimi nitachagua Digital Media Recovery kwasababu nina Memory Card (SD Card)


2. Chagua Partition unayotaka kuifanyia Data Recovery kisha bonyeza "Full Scan"

3. Iache mpaka imalizike yenyewe
 
4. Chagua folder lenye picha zako. Ukikosa kwenye Folder la kwanza, ingia la pili au la tatu utaona picha zako

5. Chagua picha unazotaka kuzirecover kisha Double Click au Right Click
6. Bonyeza Browse kisha chagua Folder au partition ambayo unataka kuhifadhi picha zako kisha bonyeza "Save"

Tags: Jinsi ya kurudisha picha zilizofutwa kwenye computer, namna ya kurudisha picha kwenye Laptop, jinsi ya kurudisha picha kwenye dekstop, jinsi ya kurudisha picha zilizofutwa kwenye flash drive, namna ya kurudisha picha zilizofutwa kwenye hard disk, jinsi ya kurudisha picha zilizofutwa kwenye memory card, namna ya kurudisha picha kwenye computer, jinsi ya kurudisha picha kwenye flash drive, namna ya kurudisha picha kwenye hard disk, jinsi ya kurudisha picha kwenye memory card, jinsi ya kurudisha image zilizofutwa, sofware nzuri za kurudisha picha zilizofutwa kwenye computer, program bora za kurudisha picha kwenye memory card, software bora za kurudisha picha kwenye hard disk, program bora za kurudisha picha kwenye Flash drive, data recovery software bora ya kurudisha picha kwenye computer, data recovery bora ya kurudisha picha kwenye memory card

No comments