Jinsi ya kuunlock E5573s-856 MTN itumie mitandao yote

Hii ni router inayotumia mtandao mmoja tu wa MTN kwahiyo ukiweka SIM Card ya mtandao mwingine inakuomba NCK Code

Kwa kutumia njia hii utaweza kuunlock Huawei E5573s-856 MTN na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka

Muhimu   
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa router.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hizi uta-brick router yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe router yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock router yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitawezekana

Namna ya kuunlock Huawei E5573s-856 MTN itumie mtandao wowote
1. Install Huawei Mobile Partner na Huawei DataCard Driver kwenye computer yako. Baada ya kuinstall, Huawei mobile partner itafunguka ifunge
2. Fungua router kwa screew driver, kisha gusanisha hizo point A na B kwa pamoja (usiachie) kisha chomeka router yako kwenye computer yako kwa USB Cable ikiwa haina SIM Card. Ukiingia kwenye Computer Management >>> Device Manager >>>>> Port (COM & LPT) utaona  
driver imeandikwa Huawei Mobile Connect - 3G PC UI Interface

3. Run Balong USB Downloader kisha bonyeza Detect. Utaona COM Port ya router yako imeionekana
4. Bonyeza vidoti vitatu kwenye Load
 
5. Chagua usbloader.bin kisha bonyeza Open
6. Bonyeza Load, iache mpaka imalize yenyewe
7. Bonyeza vidoti vitatu tena kwenye Load
8. Chagua E5573s usblsafe.bin kisha bonyeza open
9. Bonyeza Load, iache mpaka imalize yenyewe. Funga Balong USB Downloader
10. Utaona kwenye Computer Management >>> Device Manager >>>>> Port (COM & LPT) kuna driver hizi FC - Application Interface na FC - PC UI Interface
11. Run Universal Master Code, bonyeza Huawei, weka IMEI za router yako kisha bonyeza kwenye Calculate kupata Flash Code
12. Run Huawei E5573s-856 MTN Unlocked Firmware, bonyeza Start kisha bonyeza Next. Ikiomba Password, weka za flash code kisha bonyeza OK. Iache mpaka imalize yenyewe, ikimaliza bonyeza Finish
13. Run E5573s-856 MTN WEB UI Firmware, bonyeza Start kisha Next. Iache mpaka imalize yenyewe ikimaliza bonyeza Finish. 

Chomoa USB Cable kisha weka SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka
  Ikifail ku-run E5573s-856 WEB UI Firmware, rudia hatua namba 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8 na 9. Anza hatua namba 13 ya ku-run E5573s-856 WEB UI Firmware.

Hongera! Umefanikiwa kuunlock Huawei E5573s-856 MTN na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaotaka

Tags: Jinsi ya kuunlock E5573s-856 MTN, jinsi ya kuunlock Huawei E5573s-856 MTN, jinsi ya kufungua E5573s-856 MTN, jinsi ya kufungua Huawei E5573s-856 MTN, download firmware for E5573s-856 MTN, download firmware for Huawei E5573s-856 MTN, download E5573s-856 MTN, download Huawei E5573s-856 MTN firmware

No comments