Namna ya kuzuia matangazo ya internet kwenye simu ya Android


Unapokuwa unatumia simu kwenye internet (unaperuzi) utakumbana na matangazo mbali mbali yenye format ya Video, Picha, Animation na GIF ambayo huwa ni kero na kuna wakati yanakuwa na maudhui ya tendo la ndoa ambayo hukera zaidi. Kuna wakati hujitokeza pale unapowasha data tu kwahiyo inabidi uzime data kwanza kwasababu matangazo yamezidi. 

Haya matangazo hajitokezi kwenye browser pekee bali hata kwenye baadhi ya application ulizozinstall kutoka Google au Play Store. Kuna baadhi ya Application kwenye Play Store zimewekewa matangazo kwahiyo unapoinstall apps inabidi usome maelezo kabla ya kudownload (Contains Ads)

Mambo ya kuzingatia ili kuzuia matangazo ya Internet kwenye simu yako
1. Tumia application za kulipia (nunua Application)
2. Turn off notification na Force Stop kwenye application. Ingia Settings > Apps > chagua Application > bonyeza Force Stop > Notifications (enable Block all)

Unapoinstall application yenye matangazo huwa ipo on muda wote kwahiyo unapowasha data, huleta notification na baadhi matangazo huanza kuonekana hasa wanaoutumia Launcher zenye matangazo. Bila ku-block notification na force stop bado itaendelea kuleta matangazo na kutumia data
3. Tumia Browser zenye Ads blocker kama vile Opera Mini na Brave. Hii haizuii matangazo yanayojitokeza kwenye Application kwenye simu yako bali utazuia matangazo yanayotojitokeza kwenye browser tu

Jinsi ya kuzuia matangazo (internet Ads) kwenye simu ya Smartphone Android
Hii ni application ambayo itazuia matangazo yote yanayojitokeza kwenye simu yako ya Android.

Requirements
- Adguard Ads Blocker apk (Hii ina life time key). Utatumia miaka yote na wala haiombi key
- Simu

Njia hii utaweza kuzuia matangazo yote ya picha na video yanayojitokeza kwenye browser na kwenye applications zote kwenye simu yako
Kabla ya kuinstall Adguard apk, tembelea Savefrom uone ilivyojaa matangazo. Install Adguard kisha ingia Tvshows4mobile. Adguard itazuia matangazo yote yanayojitokeza kwenye simu yako kwa ujumla kwahiyo utazuia matangazo yanayojitokeza kwenye browser yoyote pamoja na Applications kwenye simu yako

Jinsi ya kuzuia matangazo ya internet (Ads) kwenye simu yako
1. Download Adguard na install kwenye simu yako
2. Fungua Adguard kisha bonyeza kwenye kitufe cha kijani ili kuruhusu "protection is enable"

3. Hakikisha imejitokeza alama ya ufunguo kwenye Notification ya simu yako

Kwa kutumia Application ya Adguard hautaweza kuona matangazo ya aina yoyote uwapo mtandaoni au unapowasha Data. Inafunga Matangazo ya Internet Ads ya aina yoyote

Tags: jinsi ya kuzuia matangazo ya internet kwenye simu, namna ya kuzuia matangazo mtandaoni, namna ya kuzuia matangazo kwenye browser, jinsi ya kuzuia matangazo kwenye application, Zuia matangazo ya internet kwenye simu za Android, Application bora za kuzuia matangazo kwenye simu, program nzuri za kuzuia matangazo kwenye simu, jinsi ya kuzuia matangazo ya internet kwenye smartphone, zuia website zenye matangazo, zuia blog zenye matangazo, zuia matangazo kwenye blog, zuia matangazo kwenye website

No comments