Jinsi ya kuunlock E153u-1 MTN itumie mitandao yote

Hii ni modem ya Huawei E153u-1 MTN ambayo inatumia SIM Card wa MTN tu kwahiyo ukiweka SIM card ya mtandao mwingine inakuandikia Invalid SIM Card

Kwa kutumia njia hii utaweza kuunlock modem yako ya E153u-1 MTN na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka

Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa modem yako.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hii uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe modem yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock modem yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi

Namna ya kuunlock Huawei E153u-1 MTN itumie mtandao wowotw
1. Weka SIM Card ya mtandao mwingine kisha chomeka modem yako kwenye computer
2. Install dashboard ya modem yako ili kuinstall drivers za modem yako
3. Baada ya kuinstall, itafunguka dashboard ya modem yako. Ifunge
4. Soma maelezo yaliyopo kwenye PDF kwenye File

Hongera! Mpaka hapa utakuwa umefanikiwa kuunlock E153u-1 MTN na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka.

 

No comments