Njia rahisi ya kufikisha subscribers 1000 kwenye channel yako ya YouTube
- Weka video nyingi (usicopy video za watu ukaweka, utapigwa copyright ban). Michezo, vichekezo, masimulizi ya watu n.k ila usiende kinyume na masharti na vigezo vya YouTube.
- Weka video zenye urefu zaidi ya dakika 4 na kuendelea
- Tumia vichwa vya habari vinavyovutia
Channel yangu inahusu masuala ya technolojia yaani kutoa huduma kwa watu katika kuunlock simu, modem na router kwahiyo sitegemei hasa kupata matangazo ya YouTube kutengeneza hela kwasababu unaweza kuingiza hela nje ya matangazo ya YouTube kwa;
- Kuuza huduma kama mimi ya kuunlock simu, modem & router
- Kuonesha matangazo ya watu mbalimbali kwenye video zako
- Kuonesha kazi zako kwa mfano;
A. Wewe ni fundi ujenzi, unaweka video zinaonesha nyumba ulizozijenga kwahiyo watu watapendezwa na kazi yako na wataanza kukupigia simu ili ukawajengee nyumba
B. Wewe ni Sonara, utaonesha vito vya thamani kama pete, mikufu na bangili ulizozitengeneza na watu wataanza kukupigia simu wakihitaji huduma yako
C. Wewe ni Cameraman utaweka video au picha za kazi zako na watu wataanza kukutafuta wakihitaji huduma yako
D. Unauza nguo, simu au nafaka kwahiyo utaweka video zinaonesha bidhaa zako na watu watakutafuta na kukulipa
Hii ni makala inayohusu watu wanaotaka kutengeneza hela kupitia matangazo ya YouTube. Unaweza kuchanganya maudhui mbalimbali yanayohusu michezo, afya, siasa na utamaduni na utaweza kuandika kwa lugha yoyote iwe ya Kiswahili au Kiingereza.
Kwa ulimwengu wa sasa, watu wamekuwa wagumu sana kusubscribe channel za YouTube. Mtu au watu wanaweza kuangalia video zako lakini ukaishia kupata subscribers 51 au 200 tu kwa zaidi ya miaka 4 na kuendelea na tena hakuna kuongezeka kwa subscribers.
Huyu channel yake ina miaka 5. Angalia watu walioangalia video ya kwanza na ya pili. Video ya kwanza ina Views 263 na ya pili ina Views 5500 hivi lakini mpaka sasa ana subscribers 186 kwahiyo alitakiwa awe na subribers 1000 (1k) kwa watu 5,000 walioangalia video ya pili tu. Kupata watch hours 4000 (4k) ni rahisi weka video nyingi na changanya maudhui kama wewe upo kwa ajili ya kupata hela kwa njia ya matangazo ya YouTube.
Ina Views 473 na ametoa free solution ambapo watu wengine wanauza na kupata pesa ila yeye katoa free kwa lengo la kupata subscribers wengi ila mpaka sasa tangu miezi 4 iliyopita ana subscribers 13 tu. Ili kupata subscribers inahitaji utumie akili ya ziada. Hata ungekuwa unapost video za vocha za mitandao, watu watajaza vocha kwenye simu zao na kujiunga na vifurushi lakini hawatawezi ku-subscribe channel yako.
Kupata Subscribers siyo kazi rahisi kama unavyofikiri, unaweza kufikiri nikiweka video basi watu wata-subscribe tu wanaweza ila nyakati hizi watu wamekuwa wagumu sana. Unaweza kufikisha watch hours 4000 ila kwenye subscribers unaweza usifkishe subscribers 1000 mpaka ukaitelekeza channel yako wakati kuna njia rahisi tu ya kupata 1000 subscribers kwa muda mfupi
Kwa kusoma kitabu hiki, kitakusaidia kufikisha subscribers 1000 na zaidi kwa muda mfupi na kwa urahisi. Channel yangu ina video za kawaida sana kwahiyo unaweza kujiuliza mbona ina muda mrefu lakini subscribers wachache? Njia hii sikuifahamu hapo awali kwahiyo nimeigundua mwaka 2023 mwezi wa 3 na nimeitumia miezi 3 tu na ikanipa matokeo ya 1000 subscribers kisha nikaachana nayo kwasababu sifikirii au kuwaza kupata hela kwa matangazo ya YouTube, nimejikita zaidi katika kutengeneza hela nje ya matangazo ya YouTube. Angalia Subscribers wangu ni halisi na siyo subscribers wa maroboti
Channel yangu, Bonyeza HAPA
Muhimu
Kitabu hiki kimeandikwa na timu ya Fahusvera, hairuhusiwi mtu yoyote kuchapicha tena (Editing), kuweka kwenye website au blog zingine bila idhini ya mwandishi. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa. Wasiliana na timu ya Fahusvera Call, SMS, WhatsApp au Telegram +255767434014 kwa maelezo zaidi. Haki zote zimehifadhiwa
Post a Comment