Jinsi ya kuunlock E5372 Viva itumie mitandao yote

Hii ni router inayotumia SIM Card ya mtandao mmoja tu ambapo ukiweka SIM Card ya mtandao mwingine inakuomba NCK Code

Kwa kutumia njia ya hii, utaweza kuunlock Huawei E5372 Viva na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka

Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa router yako tu.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hizi uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe router yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock router yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi

Namna ya kuunlock Huawei E5372 Viva itumie mtandao wowote
i. Run Universal Master Code kisha bonyeza Huawei, weka IMEI kisha bonyeza Calculate kupata Flash Code

ii. Run E5372 Viva unlocked firmware, Bonyeza Start, itaomba password. Weka za flash code kisha bonyeza OK. Subiri mpaka imalize kisha bonyeza Finish
iii. Chomoa router yako kwenye computer
iv. Weka SIM Card ya mtandao mwingine kisha washa router yako
v. Unganisha router yako na computer kwa WI-FI
vi. Itafunguka browser yenye address kama hii 192.168.1.1/simlock.asp kama itashindikana kufunguka copy hii address
http://192.168.1.1/html/simlockrequired.html na paste kwenye browser yoyote ile ya computer yako
   > Weka User Name na Password kisha bonyeza Log In

vii. Weka NCK Unlock Code ulizotumiwa na timu ya Fahusvera kisha bonyeza Apply.

Hongera! Umefanikiwa kuunlock Huawei E5372 Viva na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaotaka

 
Tags: Jinsi ya kuunlock E5372 Viva, jinsi ya kuunlock Huawei E5372 Viva, jinsi ya kufungua E5372 Viva, jinsi ya kufungua Huawei E5372 Viva, download firmware for E5372 Viva, download firmware for Huawei E5372 Viva, download E5372 Viva, download Huawei E5372 Viva firmware

No comments