Jinsi ya kuunlock E3131 MTN Zambia itumie mitandao yote

Hii ni modem ya Huawei E3131 MTN Zambia ambayo inatumia SIM Card wa Zantel Tanzania tu kwahiyo ukiweka SIM card ya mtandao mwingine inakuandikia Invalid SIM Card. Hii ni modem ya E3131 MTN Zambia ambayo inafungukia kwenye dashboard tu

Kwa kutumia njia hii utaweza kuunlock modem yako ya E3131 MTN Zambia na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka

Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa modem yako.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hii uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe modem yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock modem yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi

Namna ya kuunlock Huawei E3131 MTN Zambia itumie mitandao yote
1. Weka SIM Card ya mtandao mwingine kisha chomeka modem yako kwenye computer
2. Install dashboard ya modem yako ili kuinstall drivers za modem yako
3. Baada ya kuinstall, itafunguka dashboard ya modem yako. Ifunge
4. Run SBC Code Calculator, Bonyeza Huawei Tab kisha weka IMEI za modem yako ambazo ni tarakimu 15, bonyeza Calculate kupata Flash Code. Nukuu Flash Code
5. Run E3131 MTN Unlocked Firmware, bonyeza Start. Itaomba Password. Weka za Flash Code kisha bonyeza OK, iache mpaka imalize yenyewe. Ikimaliza bonyeza Finish

Hongera! Mpaka hapa utakuwa umefanikiwa kuunlock E3131 MTN Zambia na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka.
Tags: Jinsi ya kuunlock E3131 MTN Zambia, Jinsi ya kuunlock Huawei E3131 MTN Zambia, namna ya kufungua E3131 MTN Zambia itumie mitandao yote, namna ya kufungua Huawei E3131 MTN Zambia, how to unlock E3131 MTN Zambia, how to unlock Huawei E3131 MTN Zambia, Download E3131 MTN Zambia firmware, Download E3131 MTN Zambia Firmware, Download firmware for E3131 MTN Zambia, Download Huawei E3131 Firmware

Read More >>>> Namna ya kuunlock ZTE R207-z Vodacom Tanzania

No comments