Jinsi ya kuunlock Huawei E3372h-607 TTCL Tanzania

Hii ni modem ambayo imefungwa na mtandao wa TTCL Tanzania ili iweze kutumia SIM Card ya mtandao mmoja kwahiyo ukiweka laini ya mtandao mwingine inakuomba SIMLOCK Code.

Kwa kutumia njia hii utaweza kuunlock Huawei E3372h-607 TTCL Tanzania na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka.

Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa modem.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hizi uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe modem yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock modem yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi

Namna ya kuunlock Huawei E3372H-607 itumie mitandao yote
1. Chomeka modem yako kwenye computer ikiwa na SIM Card ya mtandao mwingine. Install Huawei driver


2. Run Universal Master Code calculator. Bonyeza kwenye Huawei Tab kisha weka IMEI namba zipo tarakimu 15. Kuzipata, Funua mfuniko wa modem yako utaziona. Bonyeza Calculate kupata Flash Code

3. Run Huawei E3372h-607 TTCL Unlocked Firmware. Bonyeza Start.

4. Itakuomba Password. Weka Flash code ulizozipata kwenye hatua namba mbili kisha bonyeza OK. Iache mpaka imalizike. Ikimaliza bonyeza Finish

5. Run Huawei E3372h-607 TTCL WEBUI Unlocked Firmware kisha bonyeza start. Iache mpaka imalizike. Ikimaliza bonyeza Finish

Hongera! Umefanikiwa kufungua modem yako ya Huawei E3372h-607 TTCL Tanzania na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote

Read more >>> Namna ya kuunlock M028AT TTCL Tanzania Itumie mitandao yote

No comments