Jinsi ya kuunlock Huawei E3372h-153 4G LTE Hilink itumie mitandao yote

Hii ni modem ambayo imefungwa ili uweze kutumia SIM Card ya mtandao mmoja na ukitaka kutumia laini ya mtandao mwingine inakuomba SIMLOCK Code.

Kwa kutumia njia hii, utaweza kufungua modem yako ya Huawei E3373h-153 4G LTE na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule.

Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa modem.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hizi uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe modem yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock modem yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi

Namna ya kuunlock Huawei E3372h-153 itumie mitandao yote
1. Chomeka modem yako kwenye computer ikiwa na SIM Card ya mtandao mwingine. Ikifunguka browser, ifunge. Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye USB Port kwenye computer yako.
2. Install Huawei DriverSetup na FcSerialDrv kwenye computer yako ili kupata drivers za modem yako

3. Run Huawei Master Code Calculator, Bonyeza kwenye Huawei Tab, weka IMEI za modem yako kisha bonyeza kwenye Calculate kupata Flash Code


4. Run Huawei E3372h-153 downgrade firmware. Bonyeza Start. Ikiomba Password, weka za Flash Code ulizozipata kwenye Huawei Master Code Calculator Hatua namba 3 kisha bonyeza Ok. Iache mpaka imalize yenyewe, ikimaliza bonyeza Finish

5. Run DC Unlocker 2 Client as administrator. Bonyeza kwenye magnifying glass. Utaletewa taarifa za modem yako. Mwisho mwa hizo taarifa, weka hizi code AT^NVRDEX=50503,0,128 kisha bonyeza ENTER kwenye keyboard ya computer yako.

Ikigoma, fanya hivi
- Funga Huawei mobile partner dashboard
- Funga Tab ya Huawei dashboard kwenye browser yako
- Chomoa modem yako kwenye computer kisha chomeka tena. Endelea na hatua namba 5

6. Utaletewa NV Harsh code. Kama hivi

Nitumie NV Harsh Code kwa SMS, WhatsApp & Telegram +255767434014 kupata NCK Code

7. Run Huawei E3372h-153 Upgrade firmware. Bonyeza Start, Next kisha iache mpaka imalize. Bonyeza Finish

8. Chomoa modem yako kwenye computer. Weka SIM Card ya mtandao mwingine kisha chomeka kwenye computer

9. Itafungua browser yenye address hii "192.168.8.1"
10. Weka User name na "Password" kisha bonyeza "Log In" ambazo ni admin kwa zote

11. Weka NCK code ulizotumiwa na timu ya Fahusvera kisha bonyeza "Apply"

Hongera! Umefanikiwa kuunlock Huawei E3372h-153 4G LTE na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaotaka

Tags:  Jinsi ya kuunlock Huawei E3372h-153 4G LTE Hilink itumie mtandao wowote, namna ya kuunlock E3372h-153 4G LTE Hilink itumie mitandao yote, jinsi ya kuunlock E3372h-153 itumie mitandao yote, namna ya kuunlock Huawei 4G LTE E3372h-153 Hilink itumie mitandao yote, namna ya kufungua E3372h-153 4G LTE Hilink itumie mtandao wowote, how to unlock E3372h-153 4G LTE Hilink, how to unlock Huawei E3372h-153 4G LTE Hilink, how to unlock E3372h-153 Hilink, how to unlock 4G LTE E3372h-153 Hilink, how to unlock E3372h-153, namna ya kufungua modem ya E3372h-153 4G LTE Hilink itumie mitandao yote, jinsi ya kuunlock modem ya Huawei E3372h-153 4G LTE Hilink itumie mitandao yote

No comments