Jinsi ya kuunlock Huawei E3531s-1 Hilink Airtel Tanzania
Hii ni modem iliyofungwa ili iweze kutumia SIM Card ya mtandao mmoja tu kwahiyo ukitumia SIM Card ya mtandao mwingine inagoma kusoma na inafungua dashboard ya kukutaka uweke SIMLOCK Code ila ukiandika haikubali.
Hii ni njia rahisi ya kuunlock modem ya Huawei E3531s-1 Hilink na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote.
Muhimu
Hii modem ni Hilink na port zake zimefungwa kwahiyo ukirun DC Unlocker Client as administrator kisha ukabonyeza kwenye Magnifying Glass, inaleta ujumbe wa Modem not found. Inabidi uifanye modem yako iweze kuonesha port ili uweze kuunlock. Jinsi ya kuwezesha port za Huawei E3531s-1 Hi-link ziweze kusoma kwenye computer yako
Modem hii, firmware yake version inaanzia na 22 kama modem yako inasoma 21 basi hiyo ni siyo Hilink na njia hii haikufai. Hii ni njia kwa ajili ya modem yenye firmware version 22 tu ambayo ni Hilink na inafunguka kwenye browser yaani kwenye Chrome, Mozilla, Opera na browser zingine.
Ili kujua unatumia Firmware Version ya ngapi. Download DC Unlocker 2 Client kisha Run as administrator. Kisha bonyeza Magnifying Glass. Utaletwa taarifa za modem yako. Angalia kwenye Firmware
Zingatia
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa modem.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hizi uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe modem yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock modem yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi
Namna ya kuunlock Huawei E3531s-1 Hilink Airtel Tanzania itumie mitandao yote
1. Chomeka modem yako kisha ingia kwenye Control Panel >>> Programs >>> Uninstall a program kisha uninstall hizi program kama zinavyoonekana kwenye picha
2. Run DC Unlocker as administrator kama inavyoonekana kwenye picha kisha bonyeza Magnifying glass button kupata taarifa ya modem yako
3. Fungua folder la Huawei E3531s-1 Hilink Firmware kisha run hiyo firmware. Ikileta error, rudia hatua namba mbili
4. Fungua Huawei Universal master code calculator. Bonyeza kwenye tab ya Huawei. Weka IMEI namba ambazo zipo tarakimu 15 (Kuzipata fungua mfuniko wa modem yako), kisha bonyeza Calculate kupata Flash Code
5. Run Huawei E3531 Update Wizard - Firmware. Bonyeza Start, ikiomba password. Weka za flash code kisha bonyeza OK . Isipoomba password usihangaike kufungua Huawei Code Calculator. Ikimaliza, bonyeza Finish6. Run Update WEBUI Unlocked Firmware
7. Bonyeza Start. Iache mpaka imalize kuinstall WEBUI Unlocked Firmware. Ikishamaliza itafungua browser yenye address 192.168.1.1 au 192.168.8.1
8. Fanya Setting upya kwenye dashboard ya modem yako kwenye web. Ingia Settings >>> System >>> Reset Settings >>> Mobile Connection Settings
kwenye shutdown interval weka 120 kisha bonyeza Apply.
Ingia Profile Management, bonyeza Create a new profile kisha andika kama inavyoonekana kwenye picha.Kisha bonyeza Apply button kusave changes
Run DC Unlocker Client as administrator kisha bonyeza kwenye Magnifying Glass button kupata taarifa za modem yako. Angalia kwenye Sim lock status itakuandikia Unlocked
Ikigoma, fanya hivi
- Funga Huawei mobile partner dashboard
- Funga Tab ya Huawei dashboard kwenye browser yako
- Chomoa modem yako kwenye computer kisha chomeka tena. Endelea na hatua namba
Mpaka hapa utakuwa umeweza kuunlock modem yako ya Huawei E3531s-1 Airtel na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote
Post a Comment