Namna ya kurudisha Data zilizofutwa kwenye Computer, SD Card, Flash Drive & Hard disk

Hii ni njia rahisi ambayo itakusaidia kurudisha data zako kama vile Video, Picha, Music, Document (PDF, DOC) n.k zilizofutwa au kuharibiwa na virus kwenye computer, Hard disk, Flash Drive au Memory Card hata kama ulizifuta kwa kubonyeza ctrl + shift (formart). Hii ni njia nyepesi ambayo mtu yoyote anaweza kuitumia hata kama hana ujuzi wowote wa computer

Data zinaweza kufutwa kwa bahati mbaya au makusudi kama vile umepiga windows halafu umesahau kuhamisha data zako kwenye Local disk C au zimeliwa na Virus kwahiyo uwezekano wa kuzirudisha ni 100%. Usiwe na wasiwasi kuhusu kutorudi kwa data zako hata kama kwenye Recycle Bin zimeshafutwa. Utazipata kwa 100%

Mambo ya kuzingatia ili kurudisha Video, Music, Picha, Document (PDF, DOC) n.k kwenye Computer, SD Card, Flash Drive & Hard disk

1. Usiweke files tena kwenye Hard disk, Flash Drive, Computer au SD Card ambayo data zimefutwa kwasababu kadri unavyoweka file mpya zinaenda ku-overwrite data zilizopo. Kama Data zilifutwa halafu ukaitumia Computer, Hard disk, Flash Drive au Memory kuweka file zingine uwezekano wa kupata Data zako ni 80%.
2. Usiifungue Computer, Hard disk, Flash drive au SD Card. Kama Hard disk haisomi baada ya kuanguka, fungua huenda kuna pin imeachia.
3. Usiitumie Flash drive, SD Card au Hard disk kwenye computer yenye virus. Data zako utazipata lakini kwa 88% kwahiyo watoe virus kwanza kwa kutumia Antivirus yeyote yenye nguvu
5. Kama ni data zilizofutwa zipo kwenye computer Local disk C, usipige windows tena. Kama zipo partition nyingine piga windows kama unahitaji
6. Uwe na hard disk au Flash drive nyingine kwa ajili ya kuwekea data zako kama data zako zilizofutwa zipo kwenye computer. Unapofanya Data Recovery kwenye computer, data zako unatakiwa uzihifadhi kwenye Flash drive au Hard disk. Kama zimefutwa kwenye hard disk, Flash Drive au SD Card ziweke kwenye computer au kwenye devices yoyote tofauti na ile unayotaka kuifanyia Data Recovery

Kuna software nyingi ambazo zinaweza kurudisha data lakini yenye uhakika wa kurudisha data zako kwa 100% ni "Hetman Data Recovery". Hii ni software nzuri kwangu na nimeitumia kurudisha Data zangu.

Mahitaji
- Hetman Data Recovery
- Flash Drive, External Hard disk, au SD Card kama Data zimefutwa kwenye computer
- Computer kwa ajili ya kuinstall Hetman Data Recovery Software

Jinsi ya kurudisha files au folder zilizofutwa kwenye Computer, Flash Drive, Hard disk au SD Card (memory card)

1. Fungua Hetman Data Recovery. Chagua Partition au Flash drive, Hard disk, au SD Card unayotaka kuifanyia Data Recovery

2. Double click au Right Click kwenye partition unayotaka kuifanyia data recovery kisha Bonyeza "Open"

3. Weka "Full analysis (searching for any available information)". Hakikisha zimewekea tiki zote kama zinavyoonekana kwenye picha. Bonyeza "Next"

4. Itaanza kuscan folder kwenye partition kwahiyo iache mpaka imalize na italeta ujumbe "Finish". Bonyeza Finish

5. Chagua Folder ambalo kuna data zako. Ukikosa kwenye folder moja angalia folder la pili au la tatu

6. Double click kwenye file au files unazotaka kufanya data recovery. Chagua Save to Hard disk au kama una DVD chagua Burn to CD/DVD kisha bonyeza "Next" Data zako utazikuta kwenye Computer yako au External Hard disk au flash drive .


Muhimu
Kama SD Card yaani Memory Card ipo kwenye simu, itoe kisha tumia TransFlash Adapter yoyote hata Modem pia.

- Jinsi ya kurudisha file zilizofutwa kwenye kwenye Computer, SD Card, Flash Drive & Hard disk
- Jinsi ya kurudisha picha, video, music doc zilizofutwa kwenye Computer, SD Card, Flash Drive & Hard disk
- Jinsi ya kurudisha folder lililofutwa kwenye Computer, SD Card, Flash Drive & Hard disk

Tags: Jinsi ya kurudisha data zilizofutwa kwenye computer, namna ya kurudisha data zilizofutwa kwenye memory card, jinsi ya kurudisha data zilizofutwa kwenye Hard disk, namna ya kurudisha data zilizofutwa kwenye flash drive, jinsi ya kurudisha data zilizofutwa kwenye Laptop, namna ya kurudisha data zilizofutwa kwenye desktop, namna ya kurudisha file zilizofutwa, jinsi ya kurudisha document zilizofutwa, rudisha picha zilizofutwa, rudisha muziki zilizofutwa kwenye kifaa chako, rudisha Audio kwenye kifaa chako

No comments