Jinsi ya kuunlock E3372h-153 MTN itumie mtandao wowote

Hii ni modem iliyofungwa ili itumie mtandao mmoja tu wa MTN kwahiyo ukiweka SIM Card ya mtandao mwingine inakuomba SIMLOCK CODE

Kwa kutumia njia hii, utaweza kuunlock modem yako ya E3372h-153 MTN na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka

Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa modem.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hizi uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe modem yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock modem yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi

Namna ya kuunlock Huawei E3372h-153 MTN itumie mtandao wowote
1. Chomeka modem yako ikiwa na haina SIM Card kisha install Huawei DataCard Driver na Mobile Broadband HL Service, ikifungua browser ya modem yako ifunge.

2. Run Universal Master Code, weka IMEI ya modem yako ambazo zipo digits 15 kisha bonyeza button ya Calculate ili kupata Flash Code. Kumbuka hapa tunahitaji Flash Code

3. Run E3372h-153 MTN Downgrade unlocked firmware. Bonyeza Start, Itakuomba password, weka za flash code kisha bonyeza OK. iache mpaka imalize. Ikimaliza, bonyeza Finish
4. Run DC Unlocker as administrator, Chagua "Huawei modems" kwenye Select Manufacturer na "Auto Detect" (Recommended) kwenye Select model kisha Bonyeza Magnifying Glass button.

Italeta details za modem yako ya Huawei E3372h-153 MTN. Hakikisha zimetokea kama hazijatokea rudia hatua upya na hakikisha hakuna kifaa kingine ulichochomeka kwenye computer yako zaidi ya modem yako ya E3372h-153 MTN 

5. Utaletewa taarifa za modem yako. Mwisho mwa hizo taarifa, weka hizi code AT^NVRDEX=50503,0,128 kisha bonyeza ENTER kwenye keyboard ya computer yako.
Ikigoma, fanya hivi
- Funga Huawei mobile partner dashboard
- Funga Tab ya Huawei dashboard kwenye browser yako
- Chomoa modem yako kwenye computer kisha chomeka tena. Endelea na hatua namba 4

6. Utaletewa NV Harsh code. Kama hivi

Nitumie NV Harsh Code kwa SMS, WhatsApp au Telegram +255767434014 kupata NCK Code

7. Run E3372h-153 MTN Upgrade Firmware kisha bonyeza start >>> Next. Ikimaliza bonyeza Finish
8. Chomoa modem yako kwenye computer. Weka SIM Card ya mtandao mwingine kisha chomeka kwenye computer

9. Itafunguka browser yenye address hii "192.168.8.1"

10. Weka User name na "Password" kisha bonyeza "Log In" ambazo ni admin kwa zote

11. Weka NCK code ulizotumiwa na timu ya Fahusvera kisha bonyeza "Apply"
Hongera! Umefanikiwa kuunlock Huawei E3372h-153 MTN na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaotaka

 
Tags: Jinsi ya kuunlock E3372h-153 MTN itumie mtandao wowote, namna ya kuunlock Huawei E3372h-153 MTN itumie mitandao yote, namna ya kufungua Huawei E3372h-153 MTN, jinsi ya kufungua E3372h-153 MTN, jinsi ya kuunlock Huawei E3372h-155 itumie mitandao yote, namna ya kuunlock E3372h-155 itumie mtandao wowote, how to unlock Huawei E3372h-153, how to unlock E3372h-153 MTN, how to unlock E3372h-153 MTN, how to unlock Huawei E3372h-153 MTN, download Huawei E3372h-153 MTN firmware, download E3372h-153 firmware, jinsi ya kuunlock moden ya MTN E3372h-153 itumie mitandao yote, namna ya kufungua modem ya E3372h-153 itumie mitandao yote

No comments