Jinsi ya kuunlock Huawei E173u-2 itumie mitandao yote
Kwa kutumia njia hii utaweza kuunlock modem yako ya E173u-2 na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka
Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa modem yako.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hii uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe modem yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock modem yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi
Namna ya kuunlock Huawei E173u-2 itumie mitandao yote
1. Weka SIM Card ya mtandao mwingine kisha chomeka modem yako kwenye computer
2. Install dashboard ya modem yako ili kuinstall drivers za modem yako
3. Baada ya kuinstall, itafunguka dashboard ya modem yako. Ifunge
4. Soma maelezo yaliyopo kwenye PDF kwenye File
Hongera! Mpaka hapa utakuwa umefanikiwa kuunlock E173u-2 na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka.
Post a Comment