Jinsi ya kuunlock E303Ms-2 MTN CONGO (21.158.13.00.473)

Hii ni modem ya Huawei E303Ms-2 MTN CONGO ambayo inatumia SIM Card wa MTN CONGO tu kwahiyo ukiweka SIM card ya mtandao mwingine inakuandikia Invalid SIM Card

Kwa kutumia njia hii utaweza kuunlock modem yako ya E303Ms-2 MTN CONGO na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka

Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa modem yako.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hii uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe modem yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock modem yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi

Namna ya kuunlock Huawei E303 MTN CONGO itumie mitandao yote
1. Weka SIM Card ya mtandao mwingine kisha chomeka modem yako kwenye computer
2. Install dashboard ya modem yako ili kuinstall drivers za modem yako
3. Baada ya kuinstall, itafunguka dashboard ya modem yako. Ifunge
4. Run Universal Master Code, Bonyeza Huawei Tab kisha weka IMEI za modem yako kisha bonyeza Calculate kupata Flash Code. Nukuu Flash Code

3. Run E303Ms-2 MTN Unlocked Firmware. Bonyeza Start, ikiomba password. Weka za Flash Code kisha bonyeza OK. Ikimaliza, Bonyeza Finish

4. Run Huawei Modem Code Writer. Bonyeza kwenye Please Select Com Port

5. Bonyeza kwenye Detect kisha chagua COM Port ya modem yako

6. Bonyeza Accept

7. Bonyeza Unlock Modem
 
8. Weka Unlock Code ambazo ni 8 digits kisha bonyeza OK

Hongera! Mpaka hapa utakuwa umefanikiwa kuunlock E303Ms-2 MTN CONGO na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka.

Tags: Jinsi ya kuunlock E303 MTN CONGO, Jinsi ya kuunlock Huawei E303 MTN CONGO, namna ya kufungua E303 MTN CONGO itumie mitandao yote, namna ya kufungua Huawei E303 MTN CONGO, how to unlock E303 MTN CONGO, how to unlock Huawei E303 MTN CONGO, Download E303 MTN CONGO firmware, Download E303 MTN CONGO Firmware, Download firmware for E303 MTN, Download Huawei E303 MTN Firmware
 

No comments