Jinsi ya kuunlock D-Link DWM 222 Telesol
Kwa kutumia njia hii utaweza kuunlock modem ya Dlink 222 Telesol na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaotaka
Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa modem yako.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hii uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe modem yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock modem yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi
Namna ya kuunlock Dlink DWM 222 Telesol itumie mitandao yote
1. Chomeka modem kwenye computer ikiwa na SIM Card ya mtandao mwingine
2. Italeta window mpya ikikutaka u-install dashboard, install ili kuwezesha drivers za modem yako. Ikishamaliza funga dashboard ya modem yako
3. Run D-link DWM 222 Telesol Unlocked Firmware. Itaanza kuupdate firmware kisha italeta ujumbe wa kukutaka u-install drivers. Bonyeza Yes
5. Iache mpaka imalize kisha chomoa modem yako, kisha weka SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka
Hongera! Mpaka hapo utakuwa umeweza kuunlock Dlink DWM 222 Telesol na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka
Post a Comment