Jinsi ya kuunlock Alcatel X602D Africell Uganda
Hii ni modem ya Alcatel X602D Africell Uganda ambayo inakutaka utumie SIM Card wa Africell Uganda tu kwahiyo ukiweka SIM card ya mtandao mwingine inakuomba 8 Digits NCK Code
Kwa kutumia njia hii utaweza kuunlock modem yako ya Alcatel X602D Africell Uganda na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka
Muhimu
- Hakikisha hakuna kifaa kingine kimechomekwa kwenye computer isipokuwa modem yako.
- Hakikisha computer yako ina charge 50% na kuendelea
- Usitumie Unlocked firmware tofauti na hii uta-brick modem yako. Itakufa jumla
- Usizime computer yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Usichomoe modem yako kipindi cha kurun unlocked firmware
- Soma kwanza maelezo kabla ya kuunlock modem yako
- Hatua moja ni muhimu sana, ukiruka hatua moja basi hatua nyingine haitafanya kazi
Namna ya kuunlock Alcatel onetouch X602D Africell Uganda
1. Chomeka modem yako kwenye computer ikiwa na SIM Card ya mtandao mwingine
2. Install dashboard ya modem yako ili kuinstall driver
3. Baada ya kuinstall, itafunguka dashboard ya modem yako ikiomba NCK Code. Ifunge
4. Run Alcatel X602D Africell unlocked firmware
5. Soma maelekezo yaliyopo kwenye File
Hongera! Mpaka hapa umefanikiwa kuunlock Alcatel X602D Africell Uganda na utaweza kutumia SIM Card ya mtandao wowote ule unaoutaka.
Post a Comment